Fursa

#FursaAsilia: Yajue haya kuhusu mti wa Mlonge na fursa zake za kibiashara..

By  | 

MLONGE:

Hustawi sana kwenye ukanda wa pwani wenye mvua kiasi na Joto, udongo usiotuamisha maji na usio na rutuba.

Kwa upande wa Tanzania, Wale wote waliojishughulisha na kilimo hiki wameona faida zake.

Swali je naweza kuwekeza hela zangu kwenye upandaji wa mlonge, jibu ni ndio na unaweza kutengeneza hela nyingi.

Unaweza ukatengeneza hela kwa kuuza mbegu za mlonge, chai ya mlonge, Asali ya mlonge, na Unga wa mlonge.

Kama familia yenu ina hekali nyingi za shamba, basi kilimo cha mlonge ni rahisi, nunua mbegu madukani.

Mbegu zake huuzwa kati ya Shilingi 1000-1500 kwa mbegu moja, na hekali moja huhitaji mbegu 400.

Baada ya miezi mitatu unaanza kuvuna majani ambayo ni mboga na pia ni chakula, baadaye utavuna mbegu na mti wenyewe.

Majani ya mlonge  hutumika kama chakula na dawa pia, watu wengi huhifadhi majani ya mlonge kama mboga ya baadaye.

Majani ya mlonge ni chanzo kikubwa cha virutubishi vingi sana kama vitamin C,calcium, protini, vitamin A, potassium.

Matunda mateke ya mlonge huweza kutumika kama mboga, hutayaarishwa kama maharagwe mabichi.

Mafuta yake yanatumika kutengeneza mafuta yaitwayo BODIE SELL, na katika viwanda vya urembo na madawa.

Mafuta yake pia hutumika kutengenezea sabuni, mafuta hukamuliwa kutoka kwenye mbegu kama ambavyo Alizeti hukamuliwa.

Majani ya mlonge huliwa na mifugo kama ngombe,. Mbuzi, kondoo, sungura.

Majani ya Mlonge, mbegu na magome hutumika kama tiba mbadala katika kutibu magonjwa mengi kama BP, presha, kisukari,

Mlonge, pia unaweza ukatibu pumu, kikohoz, upungufu wa kinga, shinikizo la damu, kibofu cha mkojo, na nguvu za kiume.

Asali ya mlonge inahitajika sana kwenye soko la dunia, ni bei kubwa sana kuuza, nawashaur wafugaji wa Nyuki walione.

Sehemu yote ya mmea wa mlonge ni biashara, kuanzia magome, mti, majani, mizizi na maua,

Mlonge hutumika kutibu maji kutoka kuwa machafu na kuwa masafi, Chukua majani yake katika kuyatunza maji.

Mlonge, nchini Nigeria, serikali iliingilia kati na kuanza kutangaza na kuimarisha kilimo cha mlonge.

Kwa upande wa Nigeria(Kaduna), wao wametengeneza mitambo ya maji na mbegu za mlonge hutumika kutibu maji.

Kwa Tanzania bado Kuna watu wachache wanaojihusisha na kilimo cha mlonge, Juhudi Kubwa zinahitajika Katika kuinua kilimo hiki.

Mpandaji wa miti ya mlonge ni mojawapo ya kuendeleza utunzwaji wa mazingira,

Sio kila sehemu huzalisha mlonge, hivyo bado Kuna soko kubwa la zao hili endapo Tutaamu kujikita vilivyo.

 

CREDITS TO: JALILU ZAID

Ukiniita Mtokambali bado utakua sahihi, karibu na Hili ndilo chimbo langu, Utajifunza Mengi yahusianayo na Kilimo. Kwa pamoja tuikuze mtokambali.com. Ungana nami twitter@mawere3. Siku zote "Haja ya Mja hunena na Uungwana ni vitendo"

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *